TIMES FM MATATANI KWA KUMFANYIA DIAMOND PLATNUMZ INTERVIEW

by - Thursday, March 22, 2018Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu Diamond aliyoyafanya katika kituo cha Redio cha Times jijini Dar es Salaam.
Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.


Baada ya Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kusema kwamba amesikitishwa na kauli za Diamond alizozitoa kupitia kipindi The Playlist cha Times Fm dhidi ya Naibu Waziri wake, Juliana Shonza, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki huyo aliyoyafanya katika kituo hicho.
Akiongea na mtandao wa gazeti la Mwananchi leo, Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.
Katika mahojiano hayo, Diamond alimjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutokana na Serikali kuzifungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.
Kisaka amefafanua kuwa kiutaratibu wao wanaangalia zaidi chombo ambacho wamekipa leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine.
Amesema suala hilo kwa sasa linafanyiwa kazi na kamati ya maudhui na kuahidi kulitolea ufafanuzi siku za hivi karibuni akiwataka wananchi kuwa na subira.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo DKt. Harrison Mwakyembe amesema si busara kwa Diamond kushindana na serikali endapo ana ushauri wowote ni vema akauwasilisha kwa njia sahihi na si kumshambulia Naibu Waziri kwa dharua na kejeli

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM