BABU SEA NA MWANAE PAPII KOCHA SASA WARUHUSIWA KUDAI FIDIA

by - Friday, March 23, 2018


ARUSHA: Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR) leo Machi 23, 2018 imesoma hukumu ya kesi ya rufaa ya wanamuziki, Nguza Viking(Babu Seya) na mwanaye, Johnson Nguza(Papii Kocha)

Wanamuziki hao walikata rufaa hiyo kupinga kifungo cha maisha walichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Juni mwaka 2004 baada ya kumkuta na hatia ya kunajisi na kulawiti watoto
-
Wakati hukumu hiyo ikisomwa, Babu Seya na Papii Kocha walikuwa miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya Uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017
-
Baadhi ya mawakili waliokuwepo mahakamani hapo wamesema licha ya kuwa wanamuziki hao wamepata msamaha wa rais, hukumu yao itasomwa.

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, imesema Mahakama za Tanzania zilitenda haki na kukiuka pia kwa upande mwingine katika hukumu ya Babu Seya na Papii Kocha.
-
Mahakama imewaruhusu Babu Seya pamoja na Papii Kocha kuwasilisha hoja ya kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa
-
Mfano wa haki iliyokiukwa ni kukaaa mahabusu kwa siku 4 bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea
-
Pia wawili hao waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia Watoto wale ambao upande wa Jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa
-
Maombi hayo yanapaswa kuwasilishwa ndani ya kipindi cha siku 30


You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM