FAHAMU FAIDA NA UMUHIMU WA KUJAMBA.

by - Monday, January 01, 2018

     
     Habari mpendwa subscriber wangu wa felix Tv na kama kawaida kabla ya yote nikutakie heri ya mwaka huu mpya wa 2018 na nikutakie mafanikio na uweze kutimiza yale ulioshindwa kutimiza mwaka 2017. Nikukumbushe kusubcribe katika channel yako hii pendwa ili uzidi kupata habari zaidi pale tuu zinapojitokeza. Leo katika segment ya Felix Darasa na Kali kuliko tunakuletea, Faida za Kujamba.
       Ndio nafahamu weng mnakua mnaona aibu kujamba na wengine wametafsiri kujamba kua kitendo kisicho na adabu na kuona ni nusu ya kwenda haja. Leo naomba nikubadili kidogo na nikupe sababu kadhaa zitakazokufanya ujivunie kila saa utakapojamba.
        Kijambo kimetengenezwa na nini?
   Mara nyingi kujamba hua si kitu kizuri sana kwa wanaokuzunguka ila kwako ni muhimu hasa kama unapenda kua na afya nzuri ya tumbo. Kijambo kinatengezwa na gesi mbalimbali ikiwa ni asilimia 9 nitrogen, 21 hydrogen, 9% crabon dioxide,7% methane,4% oxygen and 1%hydrogen sulfide ambayo ndo hufanya kijambo kunuka. Na hii hutokana zaidi na aina ya chakula ulichokula.
      Watu wengi hujamba wakiwa hawajijui hasa wakati wakiwa wamelala huku wengine wakijamba kwa kujitutumua mchana kweupeee. Kujizuia kujamba yaweza kuwa jambo la busara ila sio vyema kwa afya yako hasa pale kinapokuja automatic
    Hizi ni faida 7 za kujamba ambazo pengine ulikua huzijui.
kabla sijaanza kukuambia kama una kijambo em jamba kwanza kidogo alafu tuendelee.
1) Kupunguza kuvimbiwa
    Mara nyingi ulaji wa ulafi na usio na kipimo hupelekea kuvimbiwa na tumbo kujaa gesi. Kuna watu hukosea na kujitambisha pale wanapovimbiwa, lakini njia sahihi ya kudeal na kuvimbiwa ni kupitia kujamba kwani unapunguza au kumaliza kabisa gesi. Ila ushauri tuu ndugu yangu ukajifungie tuu chooni maana kama umevimbiwa alafu ukakiachia mbele ya hadhara ya watu, harufu yake ni kama mzogo wa paka.

2) Kujamba kunaweza kubalance diet yako.
    Ndio wala usishangae sana kujamba kwaweza kubalance diet yako ila hii ni kwa wale wanaofuatilia harufu za vijambo vyao. Kama ukiwa makini na vijambo vyako hasa harufu basi waweza kujua kama unapata lishe bora au la. Kama unakula sana nyama nyekundu basi kijambo chako kitanuka zaidi,  Kama unakula vyakula vyenye mafuta asili kama karanga na korosho, utajamba sawa na mla nyama ila chako hakitanuka sana.

3) Kujamba kunapunguza maumivu ya tumbo
Kama uko sehemu iliojaa watu na ukazuia kijambo, waweza kua unajiletea madhara kuliko mazuri. Kwa kuzuoa kijambo unaweza kupata maumivu ya tumbo yanayoitwa intestinal distention. maumivu haya yanaweza kua serious sana hivi kuliko kukizuia, kiachiee tuuuu. Jambo jema ni kwamba baada ya kujamba maumivu haya huisha mara moja. Kama umeshajamba na tumbo lako likaendelea kuuma basi jaribu kumassage tumbo lako. hii itasaidia hewa kuzunguka tumboni na kuondoa maumivu

4) afya ya utumbo mnene na hermorhoid
   Kama wewe ni mzoefu wa kuzuia vijambo hasa kina dada basi kuna hatari ya kupata matatizo makubwa kwenye utumbo wako mpana, pia kama unajaribu kuchakachua kijambo kilichokuja kiwe cha tofauti. Kimekuja kitu cha loud speaker wewe unataka kiwe silent au vibration. Watu wengi wanaozuia vijambo wako hatarini kupata matatizo ya hermorhoid na hata madaktari huwashauri kujamba pale wanaposkia ili kuepukana na hali hii. Japo kujamba kunaweza kua kunakera watu wengine, afya yakoni muhimu kuhusu watu watavokufikiria.

5) Kunusa kijambo chako ni Afya
Mwee Haya msiniulize tu mambo ya takwimu nimetoa wapi, maana sio kwa faida hizi. Watu wengi hawawezi kukubali kirahisi tuu lakini ukweli ni kwamba wanapenda kunusa vijambo vyao hasa wakiwa chobingo ama wamejibanza sehemu peke yao. Wanasayansi wanaamini kua kunusa kijambo ni moja ya kitu muhimu kwani Gesi aina ya Hydrogen salphide inayotengenezwa kwenye utumbo wakati wa umengenyaji wa chakula, husaidia kupunguza uharibifu wamitocondria kwenye seli zako.  Hivo kunusa kijambo chako kunaweza kukupunguzia chance za kupata magonja ya moyo na kiharusi.

6)Kujamba husaidia mtu kujua allergy mbali mbali za chakula
   Kujamba pale mwili unapotaka waweza saidia daktari kutambua kama unaalegi na chakula gani. Kujamba sana baada ya kula chakula fulani inaweza kumaanisha kua una allergy na chakula hicho. Kama utakua unafuatilia ni muda gani huwa unajamba sana unaweza kujua ni chakula gani sio kzuri sana kwa afya yako, Kama pizza au mayai.

7) Kujamba ni starehe
 Hahahah, duh haya bana, Watu wengi hujamba sababu ni moja ya tendo la starehe. na kujamba hukufanya urelax na kuwa confortable

Kama wewe unaona Aibu kujamba hata ukiwa mwenyewe basi yafuatayo ni mambo ambayo unaweza kufanya kuepuka kujamba jamba hovyo

1) Kula taratibu
2) Fanya mazoezi mara kwa mara
3)Epuka Carboneted drinks na vinywaji vyenye ladha za kutengeneza
4)hakikisha hauna tatizo lolote linalofanya gesu kujaa tumbni. Hapa itabidi dokta ahusike.

Asante kwa kua nasi na mwisho wa somo hili ndo maandalizi ya somo lingine ila kabla hatujakuaga tunaomba utuandikie kwamba je unadhani kujamba nitendo la aibu? Pia kama unaweza tuambie unahisi ingekuaje kama kujamba ingekua jambo la kawaida tuu?

asante kwa kua nasi nikutakie utazamaji mwema wa vipindi vinavyokuja na vilivopita share pia na marafiki

SUBSCRIBE FOR MORE. 

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM