UTATOA HUTOI HD

by - Saturday, October 21, 2017


          
          Niaje niaje wana jamvi, ni poa sana eeeh, habari za mchana. Kama kawa mi hua ni mzee wa matukio na maisha yangu yangeweza kua bonge moja la movie ila poa tuu kipaji cha kuigiza sina so nitaendelea kuwasimulia kama kawaida. Hii ilimkuta my best friend wakati nasoma chuo kule Nairobi na yaweza kua somo kwako pia em fatilia. kwa story tamu zaidi ingia hapa
          Siku moja rafiki yangu alirudi chuo akiwa kachanganyikiwa sana na anaongea kama anataka kutokwa na roho. Alikua akilalama kwamba kaibiwa na watu na anaomba msaada hata wa nauli afike nyumbani. Sasa tukashangaa huyu jamaa na ujanja wake wote kama sungura inakuaje anaibiwa mchana kweupe? Ikabidi tumsaidie nauli akasepa na kesho yake akanipa mkanda mzima.
Story ilikua hivi
         Alitoka chuo na alishika MOI AVENUE ili kuelekea ODEON kupanda daladala. Akiwa njiani alikutana na watu watatu waliovaa simple sana kwa haraka haraka waweza wajudge kama wanafunzi. walimkaribia na kumwambia 
         
      "Buda hapa tumebeba bunduki na kukuua hatuoni noma joo, sasa chenye utafanya ni kukua tu mpole si tukimalizana na wewe utaenda kama hukukufa ila ukijitia mjuaji huwesmek."  wakati jamaa anamwambia hivo alafu akapandisha Tshirt yake na kumuonyesha Pistol Ama mguu wa kuku kwa lugha zetu mtaani.  Jamaa aliamua kua mpole sana na wakazidi kumuhoji.

      "Unaenda api buda na umekaa smart ivi unakaa uko na maparoo wazito sana ama urongo?"
      Jamaa huku akijiuma akasema Naenda tuu kuchukua MAT niende home WESTII na maparoo hata hawako na doo vile ni mik hupenda tuu kutoklezea. Basi wakazidi kwenda nae wakienda polepole huku jamaa wa pembeni akamwambia nipatie hio bag uko nayo. Don't do anything funny joo juu nitapasua iyo kichwa na uwezi amini. Basi jamaa akampatia bag pole pole tuu. Kiualisia ukiangalia ni kama wanafunzi watatu wanatembea pamoja na mmoja ameamua kumpa mwenzake bag amsaidie.

      Wakaenda wakafika mbele akaambiwa em peana simu yako. Akawapa sim na akaulizwa sema Password akasema. Akaambiwa haya sasa tupatie ile doo yote uko nayo kwa mfuko. Mfukoni alikua na kama 2000KSH akawapatia kisha wakacheki M-PESA wakakuta inahela wakamuitisha password na wakapita kwa wakala wakachomoa hela iliokuepo 13000KSH. Baada ya hapo wakapita kwenye mgahawa wakanunua chakula wakala na wao ndo wakalipa na yeye pia wakamlipia.

       Sasa wakamuuliza, Kijana tukikuachia uende utaenda kusema chochote kwa mtu yeyote? jamaa na Naapa nyingi akaahidi kutomwambia yeyote huku kichwani anapiga hesabu, wakiniacha tuu napiga UUUUUWIIIIIIII kumbe wahuni hawa "Got the situation covered, walienda nae mpaka public Bathrooms (vyoo vya kulipia) Kisha wakalipa na wote watatu pamoja nae wakaingia. kisha wakamwambia ingia huko na ujifungie ndani kisha wakatoa bunduki na kumwambia sisi tunaona kama utaenda kupiga mdomo mtaani ivo wacha tuu tukusort saii saii. Jamaa akaberg zaidi na magoti akapiga basi wakamwambia lock the door for five minutes sisi tudiscuss hapa nje..

     Jamaa akafunga mlango na dakika kumi badae baaada ya kuona ukimywa wa muda ikambidi afungue mlango na hapo ndipo mapigo yake ya moyo yalianza kudunda kama Spika mbovu. Hakuamini macho yake kilichomtokea na aliona kama ni mizinguo ila ndo ivo ashalizwa.
Laptop, simu, hard disc, begi na mapeza zikawa zimeenda tuu ivo bila hata kusema nyeeef.

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM