PROFILE PICTURE ILINIPONZA

by - Saturday, October 07, 2017


Niaje mabeste. Niko na story nataka wapa. kwanza salam then tuendelee
kama miaka mbili imepita nikiwa tuu nimechill kwa instagram mara ikaingia text FB kuchek ni manzi anakaa Wamambele. Basi fast tu kureply akanieleza jinsi amependa profile pics zangu na vile angependa tue marafiki. Nikaona si ubaya, na ni vile sasa alikua ameweka picha ingine ya kadem kasupa sana kwa profile picture kakiwa kameboost hizo boobs na ziko hot kama Entrace ya KANE WA WWE hivo sikueza jizuia.
Basi io siku ilikua poa sana na tulichat almost io usiku yote. Kesho yake naamka nakushika simu napata meseji yake ananieleza vile marehemu baba ake alikua tajiri sana ila pesa zao zote zimeshikiliwa na serikali ya UK mpaka mtu ajitokeze kudai fedha hizo. Alinambia yeye hangeweza kufanya ivo kwani alikua under age ila kama mimi ningeweza kukomboa hiyopesa basi angekuja Tanzania tuanze biashara kubwa na tuoane. Alinipea maneno zingine tamu mpaka nikashindwa kataa sasa na mimi ni tamaa ya pesa ikawa imepanda kwa kichwa sasa na nawaza vile nitaflosia marafiki zangu mtaani juu iam a boss to be.
Basi vile mi nilikubali akaniambia atampatia lawyer wake info zangu tutawasiliana. In next ten minutes nikapokea meseji kutokwa kwa jamaa muwhite na ako na suit ya black na shati nyeupe. Wallahi alikua anaonekana kama lawyer na singeweza kushtuka. Basi akaniambia nimpatie email kuna documents anataka niforwadia. Nikapeana email yangu kama kwaida na MARA PAAAAAP ikaingia email yenye ilisema kwa AC ya huyu mzee iko kama Dola Laki sita na kuitoa lazima akuje mtu aliowakilishwa na wakili huyo. Mate yakanijaa kwa mdomo, nikafunga macho nikaona vile nitabadili madem kitaa, nikawaza sasa vile madem wa FB walikua hawareply text zangu sasa wataanza nililia usiku wakitaka niwapeleke KFC au Mlimani City. Nikawaza vile nitatambia masela kitaa na izo magari nitavobadili.
Two days later Lawyer akanitafuta na kunambia alikua anaangali possibilities za mimi kwenda UK ila haitowezekana kwa itachukua mda na AC yaweza fungwa na kufilisiwa na serikali. Sasa cha kufanya mimi nitume pesa kama $1500 ya kusimamia hio kesi na pia nitume document zangu kama Birth certificate na Passport. Nilishikwa na wasiwasi na nikahoji hio pesa ni ya nini na wakati wanaweza subiri nipate hizo midola ziko kwa AC then niwapee? Ghafla yule dem akatuma messeji kwamba yeye angelipia malipo yote ila yeye yupo kambini na haruhusiwi kutuma hela popote hivo mimi nimuamini kama anavoniamini ili tufanikishe hili.

Jumatatu asubuhi saa tano na nusu mimi huyo niko Posta western union nimepanga foleni na fedha zangu za kibongo takriban milion tatu na elfu sabini tayari kutuma kwenda UK. Baada ya dakika kumi natano nilifanikisha zoezi hilo. Baada ya hapo nilimtafuta Lawyer kwa muda wa masaa mawili bila kumpata, nilikua natokwana jasho jembamba kama mchuzi wa nyanya tupu na hapa akili ikanituma nimtafute dem wangu sasa. Yeye alikua fasta kujibu na akaniambia yuko Lunch akitoka tu atampigia. Pia aliniaminisha kwamba nisiogope kabisa huenda tu yule lawyer tayari anaprocess kesi hivo niwe mpole.
Nilisubiri na kusubiri ngoja na kungoja, kurudi Facebook AC imeshafutwa na sina pengine popote pa kumpata mwana mama yule jambazi. Sasa hapo ndo nikajua ama kweli watu wasiojulikana sio lazima wawe wametumwa na THITHIEM tuu


You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM