PAMBANA NA MAKE UP ZAKO

by - Thursday, October 19, 2017

   

 Leo niwape tu story yangu long time kabla sijaoa. Kipindi naishi kisela Ghetoni pale sinza mapambano. Rafiki angu kipenzi nadhani mnamkumbuka yule aliekua amepatwa na maswaibu ya Fumanizi. kama hukusoma story yake isome hapaKipindi hicho maisha yalikua ya kujiachia sana na na sikua na kifungo chochote. Ujana mwingi ulikua umetawala. Mimi na rafiki yangu huyo ilikua ni muda sana hatujaonana na hii ni kua yeye alikua mtu wa mambo mengi sana tofauti na mimi.

      Siku moja jumamosi akanipigia simu akaniambia Mzee naja kwako kukusalimia bana hatujaonana mda. Nilitaka nimtolee nje kwani nilikua nimejipanga siku hiyo nitulie zangu tu nyumbani nisifanye chochote ila akaniambia atakua na Company (kwa kawaida yetu mi na yeye, neno company ni totoz). Nikaona si mbaya hata na hivo sijamuona beste muda wacha aibuke.
   
        Basi mwanaume huyo fasta kama kawa sipendagi ujinga mbio kufanya usafi. Usiulize kwa nini nilianza na usafi chumbani kisha nikamalizia sebuleni. Nikakimbia kwa mangi nikanunua COCACOLA, SPRITE NA FANTA yale machupa makubwa. Kwenye fridge kulikua na Juice ya matunda niliotengeneza jana yake na nyumbani kwangu mpaka sasa nina desturi ya kua na bites kama biscut, karanga na cripsi. hizi ziko 24/7 haziishagi maana napenda kula kula ovyo. Basi nikamaliza hapo nikavaa kaTshirt kangu kanakobana maana rafiki yangu afya yake mbovu mbovu basi ili hio company anayokuja nayo izimikie miBICEPS niliyoikeshea GYM nikiwa advance.
       

        nikachill zangu kwa PlayStation nawangoja waje. Baada ya lisaa na nusu nikaskia mlango unagongwa. Kuchungulia kwenye kiupenyo naona Rafki angu anataasamu nene sana. "Kwani jamaa amekuja na nyoka za pori gani"? niliwaza kichwani. Yaani kwa tabasamu aliloweka nikaona kama chumba bado kichafu kiasi. mbio nikaokota okata nguo zilikua zimeanguka anguka alafu nikaenda kufungua mlango. Kwakua warembo alokuja nao walikua wamejiegesha kwa pembeni ya mlango ikabidi nitoe uso nje kuchungulia nijionee kilichomfanya bwana mdogo atabasamu kama ameona MBINGU YA YERUSALEM.
       
        Mtume na Roho yangu, Nilikutana uso kwa uso na kitu ambacho kama nikikuelezea huezi pata picha labda ungekua pale. Tabasamu iliokua usoni mwangu iliyeyuka fasta kama Bando la HALOTEL. Nadhani mmoja alitambua kufedheheka kwangu kwani aliangalia chini kwa aibu. Hawakua wabaya kivile ila Bro, ile make up walikua wamepaka usoni ni kama nusu kilo ya unga wa ngano. Alafu walivo weusi sasa unaona kabisa  foundation imeishia katikati ya shingo na kwengine ni kama ameparara. Mdomoni wamepaka lipstick kama rangi za nyumba, Makucha ni kama wameajiriwa katika kampuni ya kukuna wale watu huotwa na vipele na hawana kucha, Nisikuadisie machoni walikuaje maana waweza kosa appetait ya kusoma hapa.
       
        Kwakususia muonekano wao na kujuta kujituma kufanya usafi kwa mbio mbio, sikusema hata karibu nilifungua mlango nikauacha tuu ivo waingie. nikampa tano rafiki angu nikaenda kukaa wakaja kila mmoja akakaa. Nikaenda kwenye fridge nikatoa masoda yote nilinunua nikaweka mezani juice na pakti moja ya kripsi alafu nikakaa zangu. wakaanza kucheka  yeye na rafiki ake wakioneshana picha instagrama huku bila huruma wakifakamia juice ambayo ilinigharimu lisaa lizma uitengeneza. Basi na mimi na rafiki yangu tukageukia TV hao kucheza Fifa.
     
    Yule mmoja aliekua karibu na mimi, ambae alikua amevaa wigi linakaa kama kileba cha ABUNUASI akaamua kuvunja ukimywa na kuniuliza,
   
      "Ferii kwani we unafanyaga nini? maana jinsi naona umenyoa hizo nywere zako si mtu ameajiliwa, unaonekana una hera ee"? (Hakuna kitu nachukia kama mtu asiejua R na L)
     
     " Yea mimi nafanya mishe zangu tuu, siko na hela kivile napata tu za kujikim on daily basis" Nilimjib short kwa sababu nilikua sina hata mood ya kuendelea kupoteza muda wangu kuongea naye.

      "Acha uongo we kaka, hivi vitu huku ndani kwako si ni ghari sana? ama umenunuriwa na wazazi wako?" Aliuliza huku akitikisa wigi lake kwa madaha.

      "Hapana nimenunua mwenyewe ila ni kwa kupigika sana asee, Kwani wewe unafanya nini?" ilibidi nibadili upepo sasa maana ilikua too much

      "Kwa sasa sina kazi ira kuna sehemu naendaga tuu kufanya Photo shoot. Nina prans za kua Moder"  Niliskia mbavu zikipasha moto na kutetemeka kama injini ya gari la mashindano tayari kwa kucheka kicheko cha mwaka. Nilijizuia kwa nguvu zote na nikamwambia kwa kifupi
     
      " nakutakia mafanikio katika hilo" nilisema hivo huku nikigeuzia attention yangu yote kwenye Play station na nikamuacha apo akinywa juice yangu kana kwamba anajua machungu nilipitia kukatakata izo machungwa.

      Baada ya muda mfup nikaanza kusikia kama rato zinanikwaruza kwenye Biceps zangu na kuangalia ni hii mwanamke ilikua inanishikaka na makucha zake, Nilijiskia ni kama nimeshapata tetenus na sasa nikuacha wosia tu ndo imebaki, wakati nawaza ikaskika sauti akisema

        "Guys hamskii njaa? si tununueni PIZZA ture?"
       
        Nikamgeukia kwa upole na sauti ya kiutamaduni nikamuuliza, "  UNANUNUA WEWE?"

       Dada huyu aliniangalia kwa macho makali yenye kupigwa na butwaa basi na sura yake ilivokua nikaona kama natazamana uso kwa uso na wakili wa SHETANI. Hakuamini kama ni mimi ndo nimeuliza swali lile
       
         "Yaani Ferix hizo hera zote unashindwa kutoa hapo erfu alobaini tuu ununue pizza ture? we mwanaume mchoyo wewe khaa?"

           nikasikia ni kama mtu amenishika koromeo nisiheme, nikikumbuka na jinsi amefanya madhambi kwenye Biceps zangu na makucha yake basi hasira ikapanda zaidi, nikatokwa povu la karne. na mwisho nikasema, Kuna juice io apo mnywe mtu akiona hawezi kunywa juice peke yake amezee na soda mkimaliza mchanganye kwato na muende mkale pizza kwenu. wakanyanyuka kwa hasira na wakaenda nikabaki na rafiki angu tukiwaza vile mipango imeenda kombo.

       ila hakikuaribika kitu tulimalizia mechi moja yeye akaenda kwao na mimi nikapigia sim kachenchede kangu ka wakati huo kakaibuka kwa nguvu ya soda na MARA PAAAAP machungu ya kuwaona MAVEMPAYA wakinywa juice yangu yakapotea.

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM