KUNGURU MWOGA HUKIMBIZA MBAWA ZAKE

by - Thursday, October 19, 2017

  
     Kwa kawaida wanawake wanapenda sana kuingejiwa na wanakuaga na mbwembwe hao. Akishavalishwa pete basi kila siku atakua anajidai anapost kucha zake snapchat kumbe tu anataka muone kapete kake na yeye kavalishwa. wengine wana vidole kama pingili za miwa ila kupost hawaachi. Yaani unakutana na mtu kapost picha ya engagement yake unajiuliza "kwa ni hii pete ina zipu au kifungo?" maana ukiwaza ameivaaje na anaivuaje hupati majibu. Mtoto wa kike ana nuckles kama Drumstick za kuku wa kienyeji? mweee


     ila sio kesi dada huyo hapo kwenye video sijui ni ushamba au ndo ile kusema haka ni kabuzi tu nakachuna mpka kieleweke?  Mwanaume kajiumua kanunua Pete alafu kwa utaratiibu kapiga magoti kama anasali kitubio na kutoa pete. Mwee bi dada kageuka Hussein Bolt kwa kasi ya 4G yaani ni nduki

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM