KONYAGI EXPRESS

by - Friday, October 20, 2017

      TRUE STORY ambayo ilinikuta utotoni kabisaa nikiwa kwetu kijijini. Kwanza kabisa niweke sawa jambo moja, kwa tambo zangu na mbwembwe wengi mnaweza kuzani mimi ni mhaya ila mimi ni MCHAGGA pure tena chronical.


Habarini za leo wadau wangu kama kawa ni siku nyigine tena tunakutana hapa hapa katika simulizi mororo ila leo nawaletea
       Nikiwa uchagani enzi za utoto wangu nilikua mtundu sana na sio siri nilikua nampa sana headache bibi yangu. Nilikua kipenzi cha babu na kati ya wajukuu waliokua karibu yake i was in the front line. Sasa kule kwetu kipindi hicho nakua umeme kulikua hamna na tulikua tunatumia Chemli nadhanni (wengi mnazijua kama hujui chemli kagoogle) basi kama wengi mnavojua chemli hutumia mafuta ya taa. Dukani mafuta ya taa hupimwa na kidude flani cha bati ila vibebeo maarufu vya mafuta ya taa vilikua ni vichupa vidogo vya KONYAGI.
       Siku moja Marehemu shangazi yangu (May she RIP) alikua nje mida ya saa moja anaweka mafuta kwenye chemli na akaweka kidogo sana na kuacha kichupa hicho kimejaa karibia robo tatu. Nikiwa na umri wa miaka mitano tuu nilitoka huko nilikotoka nikakuta chupa ya Konyagi imekaa kihasara hasara mi nikajua ndani kuna MACHOZI HAYO YA SIMBA.  Bila kuionea huruma wala aibu konyagi ile niliinya kama nakunywa maji ya Chemchem ya uzima. Niliimiminia mdomoni kama Mmeru Muuza maziwa anavomimina maziwa kwenye sufuria nikaficha chupa chini na kukimbia.
       Sikuwahi kunywa konyagi nijue ina ladha gani, Pia sikuwahi kunywa mafuta ya taa pia. Mimi nilijiridhisha kwamba nimekunywa konyagi chupa nzima na niko fiti. Haikuchukua dakika tatu nikaanza kusikia kama WCB wanaperform ZILIPENDWA huku tumboni kwangu. Yaani ilikua ni Bruuu Briiii Broaaaa. Nikaita bibiii akaja fasta nikamwambia,
             "nimekunywa konyagi saivi tumbo linaniuma"
           
             "Konyagi? umetoa wapi?" aliuliza bibi kwa mshangao sana
   
      Marehemu shangazi alikua pembeni na aliskia nikijibu kua ilikua kichanjoni pale nyuma ya jiko basi akajua wooo ili FALA limekunywa ile mafuta ya taa yote na kwa haraka akamwambia bibi "LIMEKUNYWA MAFUTA YA TAA" Basi sitosahau bibi alitoka mbiombio na kuwahi jikoni ambapo ndo mifugo pia ilikua akakamua maziwa ya ng'ombe fasta akaniletea nikagigida kama akili imeruka CM kadhaa na nikaanza mkutapika. Sasa hapo mi nikageuka Gari la matapishi maana na maisha ya kijijini tena kula kula ilikua tabia yangu yaani sikai bila kupakia machakula.

          Nakumbuka nililala siku tatu mwili umelegea kana kwamba ni mtu alinilegeza bolt za viungo. Basi tangu skuio mpaka nafika miaka 19 ndo nilishika tena kilevi. Saivi konyagi naitandika kisawasawa tena inanipa machungu nikikumbuka nilivougeuza mwili wangu chemli basi ninapata hasira za kuongeza BAPA TUU
    

          Anyways kitaani kwetu konyagi inaitwa BAPA, Nguvu za Kiume au MUA. Je kwenu             mnaiitaje pombe hii ambayo nusura initoe roho?

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM