KIFO CHA MENDE.

by - Wednesday, October 18, 2017


Habari za leo ndugu zanguni ni matumai mu wazima wa afya na kama kawaida mnapambana na hali zenu kama inavopasa. Baada ya kupambana na hali yangu kwa muda mrefu nikaona sio vibaya nikienda kijijini kuwasalimu wazee. Nikisema wazee namaanisha Babu na Bibi maana mimi Baba na Mama ni wa hapahapa mjini tunapishana Kkoo kila weekend.

Katika safari yangu ya kule kama kawaida niliinjoy kaubaridi ka kule na kwa wale wenzangu na mimi wa kupiga chupa moja au mbili unapokua likizo basi nadhani unatambua raha ya kuchapa bia kwenye baridi. Kwa kweli naweza sema niliinjoy kwa kiasi kikubwa ila balaa lilikuja sasa juzi wife aliponiomba nipitie kwao (ukweni) wanazawadi wanataka kumpa ikiwa ni pamoja na ndizi na maharage.
Kwao na kwetu ni majirani ni kama nyumba sita zinatutenganisha na kwakweli wazee wake na wangu walikua hawapatani ila mahusiano yangu na yake ndo yaliwapatanisha wazee hao. Babu alitaka kwenda namimi ila kwa kua ni mgonjwa mgonjwa nikamshauri abaki tu nyumbani nitawwasilisha salamu zake. Mtoto wamjini navopenda tambo nikangurumisha mgari wangu huyo kuenda nyumba ya jirani ambako ningeweza tu kutembea.
Kufika nikawakuta wananingoja na kama kawaida wazee wetu wakifika umri flani wanakua na adabu kuliko sisi. walinikaribisha kwa heshima zote na wakaniuliza nakunywa nini. Kwakua niko ukweni ikabidi nivae ngozi ya kondoo kwa muda na nikasema naombeni maji tuu. Dada ake wife ambae nilisoma nae hapo kijijini na nilikua namnyemelea wakati tuko shule ndo alitumwa kuniletea maji na akarudi akisema maji ya kunywa yameisha labda anipatie chai. Basi nikamwambia leta.
Basi nikaletewa Thermos na kikombe na nilivomimina chai ile kama imepimwa vile ilitoshea kikombe kimoja cash. basi nikaanza kunywa huku tunapiga story. Cha ajabu chai ile ilikua na kama mafuta na nikachomekea kijanja swali na jibu nikapewa kua Ng'ombe skuizi wana afya sana hivo hata maziwa yao yana mafuta.
Basi chai inavozidi kuisha inazidi kua tamu na mafuta yanazidi. Kwa kua ilikua mwisho mwisho nikaanza kumeza machicha hivo ikabidi nitumie meno kama chujio kuchuja chai ile. Ile namalizia kuangalia ndani ya kikombe ASTAGHFIRULLAH nikakutana na Mende wa makamo. Yaani mende huyo kwa haraka haraka alikua amekula chumvi nyingi asee maana alikua na ukubwa ambao si wa kawaida. Kucheki vizuri sehemu yote ya tumbo kulikua hamna kitu na hapo akili ikanituma yale mafuta niliokua nasisimka nikimeza. 
Niliaga kwa adabu na mapema kukimbia nyumbani gari ilibidi niiache kwanza pale ukweni niliiendea jioni. Kwa muda wa kama masaa manne nilikua napiga Konyagi na Maji tu iikudilute mafuta ya mende Tumboni.
https://goo.gl/7u6Bz7

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM