BADAMU BATAMWAGIKA

by - Thursday, October 19, 2017


Juzi kati rafiki yangu wa karibu sana ambaye naweza sema ni ndugu yangu kutoka na urafiki wetu wa muda mrefu alikutwa na maswaibu ya kusikitisha kidogo ambapo nimeona niwashirikishe wanajamvi humu ili yasije wakuta.

Miezi kama mitatu iliyopita jamaa alikua anatoka DSM anarudi zake arusha kwa ajili ya kuendelea na Kazi zake na alipanda basi aina ya DarExpress pembeni yake alikaa mrembo mashallah ambae yuko kama mid 20's wakapiga story na contacts wakapeana. nakumbuka jamaa alivofika chuga aliniadisia mpango mzima na kunambia walikua wamepanga kwenda kuchubuana weekend inayofuata.

Siku tatu badae demu alimwambia jamaa kua anarudi dar wamepata msiba na demu alikaa kama miezi miwili. Kurudi arusha akamtafta jamaa na wakapanga tena kwenda kudundisha tenesi na ndipo mchuzi ukaingia Kinyesi.


Ndani ya chumba cha hotel mwanamke alikua anatetemeka na anasita kabisa kutoa mavituzi. jamaa akaanza kubembeleza na kubusubusu mara huku kule Jamaa anasema 
alitumia kama dakika kumi natano kumshawishi tu binti yule avue kifuniko chake cha asali, basi ikawasasa season 2 kumpanga sasa ili aweze kutumbuiza.

Mara binti aombe kwenda chooni, mara badilisha channel mara sijazoe kufanya hivi vitu na story kibao ila baada ya nusu saa kukatika mlango uligongwa na kuuliza ni nani ikaskika sauti ikisema, muhudumu njoo usign. Jamaa akasema si nimeshasign ila akaambiwa daftari lingine lile silo.

Kufungua mlango akakuta vijeba watatu wameshika majambia (Masime) na wakamwambia ukipiga kelele tunakata Jojoleo. jamaa akawa mpole na akarudi zake ndani kusikilizia kitakachoendelea.

Baaada ya ukimywa wa kama dakika tano jamaa ikabidi aulize jamani kwani kuna nini na nyie kina nani? mmoja wao akajibu "we si ndo kijeba wa kula wake za watu sasa leo utaeleza maana mke wangu najua mateso nayopata nae, juzi nimetoka kumtibu Kisonono ulichomwambukiza" Sasa kumbe mchezo umepangwa kwamba isemekane hata sio mara ya kwanza wamekutana washawahi kunyanyuana tena.

Jamaa alipigwa na butwaa ila kwa vipande vya mtu vilivokua pale ndani ilibidi awe mpole na sasana kilichomuogopesha zaidi ni zile sime mpya. Jamaa akaambiwa sasa wewe dawa yako ndogo sana, chagua moja mapanga yachezeke hapa ndani ? au mafuta yatumike au utakabidhi pesa taslimu shilingi milion 3 kufidia gharama na faini ya kumlala mke wangu.

Jamaa kwa muda huo hakua na kitu hivo akaomba kuomba kwa ndugu na akaruhusiwa na simu yakwanza akapiga kwangu. Kwa kweli mimi nilikua vibaya sana na nilimuahidi kumkopa milion 1 ndani ya siku mbili zijazo ila aliitaka siku hiyo maana alikua anashida nayo. Hakuniambia kwa wakati huo shida ni ya nini.

Kwa taarifa aliyonipa ni kwamba hakufanikiwa kupata io Milioni 3 na mpaka sasa yupo hai na hakuna jeraha lolote la kukatwa na panga mwilini mwake . sitaki kujua zaidi yaliyompata ila mi nawasihi tu Bandugu tuache twamaa demu usiemjua mwogope kama ukoma.

Bakinyeshi balimwagika

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM