KIZUNGU NI KISOMI?

by - Wednesday, September 20, 2017personal, iam not but yes because not true so we wiill yes of cause in your city here.
najua sijamaanisha chochote hapo juu ila nilikua nawaonyesha tu kwamba hata na mimi darasa la saba C wa mwaka 2007 nina vimsamiati kadhaa na vijua.


turudi kwenye mada, nilikua Ofisi flani kubwa tu ya sekirali jana na kama kawaida "zombie halishibi damu" mbele yangu alikua kasimama mtoto sio poa. mguu mguu dadeki. Sasa dada alikua anataka karatasi zake alizozifuata hapo na akawa anajiuma uma hata kujielezea hawezi. akawekwa pembeni kwanza mi nikasogea nikataja tarehe niliyopeleka document zangu na nikapewa.
sasa dada akaambiwa unaona mambo ni simple tuu. unaeleza tarehe unapewa. akaulizwa we kabila gani? akajibu muhaya sasa hapa ndo mambo yakawa kivuruga kivurugi.
dada akaulizwa sasa mbona mhaya mshamba ivo? wahaya nyie si wasomi sana jaman? ah kudadeki bidada akaanza kutema inglish sasa "iam just trying to explain to you..." jamaa akamkatisha akamuuliza, kwani nimekuambia kiswahili sikielewi? au usomi ndo kizungu?


NAMI NALETA SWALI JF, KIZUNGU NDO KISOMI?

You May Also Like

0 comments

POST ZETU ZA INSTAGRAM